Hip hop ni aina ya muziki
unaoelezea aina ya usanii na
utamaduni fulani uliyotokana na
jamii ya Wamarekani Weusi na
Walatino kunako miaka ya 1970
huko mjini New York City, hasa
katika kitongoji cha Bronx.[1][2][3]
DJ Afrika Bambaataa alieleza kwa
muhtasari wa nguzo nne za
utamaduni wa hip hop: U-MC, U-
DJ, breaking na uandikaji wa
graffiti. [4][5][6][7] Elementi
zingine ni pamoja na beatboxing.
[8]
Kwa vile imeibukia kutoka mjini
South Bronx, utamaduni wa hip
hop umeenea dunia nzima. [9]
Muziki wa hip hop awali
ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa
wanatengeneza midundo kwa
kutumia mtindo wa kurudirudia na
kusimama (hasa katika visehemu
vidogo vya muziki wa kusisitiza
mwelekeo wa kigongoma) kwenye
turntable mbili, hasa hujulikana
kama kusampo muziki.
Hii baadaye ikaja kusindikizwa na
"rap", mtindo wa wizani unaotoa
maneno au mashairi yaliyo kwenye
vipimo vya mstari ulalo wa nota 16
katika fremu ya muda, ikiwa
sambamba na beatboxing,
maujanja ya sauti hutumika hasa
katika kugezea mfumo wa midundo
na elementi za muziki mbalimbali
na mautundu na vionjo kadhaa
kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.
Muundo kamili wa kudansi na
staili kadha wa kadha za mavazi
zimezua mashabiki miongoni mwao
katika muziki mpya. Elementi hizi
zimeonesha mabadiliko ya na
maendeleo kadha wa kadha katika
historia ya utamaduni huu. Baadhi
ya miziki ya hip-Hop hutoa
maelezo ya kisiasa.
Mahusiano baina ya graffiti na
utamaduni wa hip hop unatokana
mionekano mipya tofauti
iliyoongeza ufafanuzi wa kina na
uenezi tofauti wa kivitendo
ambapo kwingine walichukulia
elementi ya hip hop kama sehemu
ya sanaa, kukiwa na mpitilizo
mkubwa baina ya hao wanaondika
graffiti na hao wanaotenda
elementi zingine za hip hop
kivyao. Leo hii, graffiti imebakiwa
kuwa sehemu ya hip hop, wakati
kwa upande wa sanaa imechukua
eneo kubwa katika masuala ya
picha na michoro katika
maeneosho mbalimbali duniani
kote.
Friday, 14 February 2014
TAMBUA MAANA YA HIP HOP NA ASILI YAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment